EDWARD Lowassa Ampongeza Rais John Pombe Magufuli
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi.Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchi Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri.
Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta.
Lowassa alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akigombea kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA.
Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.
Akielezea Opersheni UKUTA, Lowassa alisema kuwa walipanga kuandamana ili kupinga dalili za udikteta alizoanza kuzionyesha Rais Magufuli.
Master J Aliniambia Sijui Kuimba – Harmonize

Mkali wa wimbo ‘Bado’ Harmonize amefunguka na kuelezea harakati zake za muziki mpaka anafika kwenye mafanikio huku akiweka wazi jinsi alivyoambiwa hajui kuimba na Master J katika shindalo la BSS.
Muimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, amesema baada ya kuambia hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.
“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS, hata mimi ningekuwa ni jaji, ningesema wewe huwezi Walter Chilambo anaweza,” alisema Harmonize. “Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master J aliambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa Master J alinichana kabisa hajui kuimba,”
Muimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea.
“Mimi nilikuwa naimani moyoni mwangu, kwamba kuna siku Watanzani wataisikia sauti yangu, japo kuwa ukimwelezea mtu mwingine mimi nakipaji hichi, naimba anasema wewe hujui, Master akaniambia wewe hujui, lakini kwa mtazamo wake alikuwa sahihi kwa sababu the way nilivyokuwa naimba hata kama ningekuwa jaji ningejitoa. Lakini mimi moyoni mwangu nilikuwa nasema ninakitu fulani, sikukata tamaa nikaendelea kufanya muziki mzuri na kweli Mungu ameniona sasa hivi nimesikika,”
Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.
Muimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, amesema baada ya kuambia hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.
“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS, hata mimi ningekuwa ni jaji, ningesema wewe huwezi Walter Chilambo anaweza,” alisema Harmonize. “Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master J aliambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa Master J alinichana kabisa hajui kuimba,”
Muimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea.
“Mimi nilikuwa naimani moyoni mwangu, kwamba kuna siku Watanzani wataisikia sauti yangu, japo kuwa ukimwelezea mtu mwingine mimi nakipaji hichi, naimba anasema wewe hujui, Master akaniambia wewe hujui, lakini kwa mtazamo wake alikuwa sahihi kwa sababu the way nilivyokuwa naimba hata kama ningekuwa jaji ningejitoa. Lakini mimi moyoni mwangu nilikuwa nasema ninakitu fulani, sikukata tamaa nikaendelea kufanya muziki mzuri na kweli Mungu ameniona sasa hivi nimesikika,”
Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.
Ruby Akanusha Kuwa na Tattoo ya Freemason
Ruby alikanusha kuwa katika imani hiyo na kusema kila kuwa mtu ana jicho na hana maana ya kuwa kwenye imani hiyo ya Freemason bali yeye ni Mkristo na anamuamini Mungu.
“Hakuna binadamu bila macho, na mimi ni mkristo namuamini Mungu so sijawahi kuingia kwenye Freemason so hizo ni imani za watu na hiyo tattoo sijachora kwa ajili ya Freemason.” Amesema Ruby.
Pia kuhusu uongozi Ruby ameweka wazi kuwa kwa sasa anajisimamia yeye mwenyewe, “Nimeamua kubadili uongozi na sasa najisimamia mwenyewe kwa ajili ya mashabiki wangu”.
“Hakuna binadamu bila macho, na mimi ni mkristo namuamini Mungu so sijawahi kuingia kwenye Freemason so hizo ni imani za watu na hiyo tattoo sijachora kwa ajili ya Freemason.” Amesema Ruby.
Pia kuhusu uongozi Ruby ameweka wazi kuwa kwa sasa anajisimamia yeye mwenyewe, “Nimeamua kubadili uongozi na sasa najisimamia mwenyewe kwa ajili ya mashabiki wangu”.
Mtangazaji mpya wa Clouds FM, Kicheko ni jiwe lililogeuka dhahabu

Maisha ni safari na hatutakiwi kukata tamaa kwa kuwa hatujui kesho yetu. Ukiisikia historia ya maisha ya mchekeshaji ambaye kwa sasa amegeuka kuwa mtangazaji wa Clouds FM, Kicheko unaweza kutokwa na machozi kama huna uvumilivu.
Awali Kicheko alikuwa member wa Ze Comedy ya EATV baada ya kuchaguliwa kwenye shindano la kutafuta wasanii watakaogiza kwenye kipindi hicho ambapo alidumu hapo kwa muda wa miaka isiyopungua miwili.
Waswahili wanasema “acha kazi, uone kazi, kupata kazi, ilivyokuwa kazi,” lakini kwa Kicheko haikuwa ngumu kwake kuacha kazi EATV ya uchekeshaji baada ya kuchukua maamuzi ya kuandika barua ya kuacha kazi kwenye uongozi wa kampuni hiyo April, 2014 huku akiwa hana kazi. Lakini pia mtangazaji huyo amepinga taarifa za kuwa alifukuzwa kazi kwenye kituo hicho cha runinga.
Baada ya muda kupita Kicheko alifanikiwa kupata shavu la utangazaji kwenye redio ya EFM akiendesha kipindi cha Singeli ‘Genge’ ambacho kimekuwa kikipendwa zaidi na mashabiki mitaani na kufanya brand yake kuanza kuwa kubwa.
Kumbe ilikuwa ni dhahabu huku wengi wakidhani lilikuwa ni jiwe, rangi yake ilifichwa na vumbi ndiyo maana kila mpita njia alilidharau kabla ya EFM na hatimaye Clouds FM kuliokota jiwe hilo na kulisafisha na hatimaye sasa rangi yake halisi imeonekana na kila mtu ameanza kulitamani tena.
Akikaribishwa kwa mara ya kwanza leo kwenye ofisi za Clouds Media (mjengoni) kwenye kipindi cha ‘Leo Tena’ mtangazaji huyo ameelezea historia yake kidogo huku akidai kuwa aliwahi kuwa mwizi huko nyuma. “Mwanzo nilikuwa mwizi, mkabaji. Unajua haya ni maisha tu,” amesema Kicheko.
Kwa sasa Kicheko amepewa heshima kubwa na watu wa mtaani ikiwa ni pamoja na kumpa jina la ‘Rais wa Uswazi’ kutokana na support yake anayoitoa kwenye muziki wa Singeli ambao umeonekana kukubalika zaidi kwa sasa huku akiwa na wanachama 489 kwenye kikundi chake.
Mchekeshaji huyo anatarajiwa kuanza kazi kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uswazi Flava’ hapo Clouds FM.
Bongo5
Agnes Amwaga Povu Kuhusu Watu Kukosea Nguo yake Baada ya Kuonekana Akificha Kitu Sehemu yake ya Mbele!

Agnes amwaga Povu Kuhusu Watu Kukosea nguo yake baada ya kuonekana akificha kitu sehemu yake ya mbele!!! Aandika mazito na matusi juu...soma hapa..๐๐๐๐.
By @officialagnes1 - Sikien nyie makuma mnaojua kutoa kasoro za watu mbuzi nyie hamnaga kazi zakufanya kazi kufwatilia maisha ya watu humu Instagram Na kukosoa watu Cjui alie nitengenezea Nguo amekosea cjui Nguo mbaya cjui cjapendeza ckien nyie makuma nipendeze nisipendeze cjawavalia alienipa hela yanguo akinisifia bas inatosha nyie wala hamkunipa pesa ya kununua nguo sasa cjui hiyo midomo yenu inawatoka funza mpk kuongea huo ukuma wenu mbwa nyie hapo mlipo mnamaisha magumu siajabu hata I phone hamjawah kumilik mko busy na vitekno vyenu kutowa kasoro watu humu ndani siogop kuma yyt nimechoka sasa maanaemnapenda kuwapanda watu

Wanafunzi Wacharaza Viboko Walimu Wao, Mmoja Ang'olewa Meno Matano, Mwingine Ngeu Kichwani
Wawanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, wanadaiwa kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili miongoni mwao akiwemo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Makonda Ng’oka “Membele'‘ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho.Walimu hao wawili wamedai kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na wanafunzi wao wenyewe ambapo Mwalimu Gabriel Kambona aliachwa na ngeu kichwani.
Mei mwaka huu, Ng’oka “Membele” alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Novemba 2015 na Aprili mwaka huu.
Ilisemekana kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kulifuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano sasa wako Kidato cha Sita katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.
Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.
Hata hivyo, baada ya kutopatikana ushahidi wa kumtia hatiani Ng’oka, Julai 27, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda ilimwachia huru.
Mwalimu Ng’oka aliripoti kwenye kituo chake cha kazi shuleni Usevya Agosti Mosi mwaka huu ambako kurejea kwake shuleni hapo kunadaiwa kuamsha hasira kwa baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wakidai hawapo tayari kumwona mwalimu huyo na familia yake shuleni hapo.
Akizungumza na wanahabari jana mjini hapa, Ng’oka alidai kuwa hayuko tayari kuendelea kufundisha kwenye shule hiyo akihofia usalama wake na kutokana na kipigo alichokipata cha kushambuliwa na baadhi ya wanafunzi wake wa kidato cha tano na cha sita wakati akiwa nyumbani kwake na familia yake.
Akisimulia mkasa huo, alisema Agosti 12, mwaka huu usiku alikuwa nyumbani kwake shuleni hapo pamoja na familia yake pamoja na mwalimu mwenzake, Gabriel Kambona aliyekuwa amemtembelea.
“Ghafla, saa mbili usiku nikiwa maliwatoni nikioga lilitokea kundi la wanafunzi wa kidato cha tano na sita wakiwa na silaha za jadi kama vile fimbo, marungu, mawe na matofali na kuanza kuishambulia familia yangu pamoja na mwalimu Kambona,” alieleza na kuongeza kuwa alilazimika ‘kuchomoka’ bafuni baada ya kusikia mayowe yaliyokuwa yakipigwa na familia yake wakiomba msaada. Alipofika sebuleni alishuhudia wanafunzi hao wakiishambulia familia yake kwa kuwacharaza viboko.
“Ndipo walinigeukia na kuanza kunishambulia kwa kunipiga kwa marungu na fimbo hadi nikapoteza fahamu nilizinduka nikiwa nimelazwa kwenye Kituo cha Afya Usevya na kubaini kuwa nimepoteza meno yangu matano huku nikiwa nimejeruhiwa vibaya kichwani. Baadaye nilihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako nililazwa wiki moja na nusu kwa matibabu na sasa nimepewa rufaa niende Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar kwa matibabu zaidi,” alieleza.
Alidai kuwa uhasama baina yake na wanafunzi hao umedumu kwa muda mrefu, lakini anashangaa uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe na Wilaya ya Mlele umeshindwa kumpangia kituo kingine cha kazi na kuchukua hatua yoyote kwa wanafunzi hao licha ya kupeleka majina yao kwa kuwa anawafahamu wote waliohusika.
Mwalimu Kambona alidai kuwa hayuko tayari kuendelea kufundisha kwenye shule hiyo kwamba kitendo cha kupigwa na wanafunzi wake kimemfedhehesha.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, walimu wa shule hiyo waliketi baada ya kutokea kwa tukio hilo, na walifikia maamuzi kuwa wanafunzi wote waliobainika kushiriki kuwashambulia walimu wao wasimamishwe shule akidai kuwa uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe na Wilaya ya Mlele ulipinga.
“Nimeandika barua ya kuomba uhamisho kwani nia aibu kwangu kuendelea kufundisha wanafunzi ambao wamenishambulia na kunitoa ngeo kichwani ….. siku hiyo ya tukio niliibiwa simu mbili za kiganjani lakini jana nimefanikiwa kuikamata simu moja kwa mwanafunzi wa kidato cha tano anayeitwa , Alex Maiko Makona na tayari amemfikisha katika Kituo cha Polisi cha Usevya,” alidai.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Katavi, Gregori Mshota alisema tayari chama chake kimeanza kuwasiliana na uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe na uongozi wa Wilaya ya Mlele ili kuhakikisha mwalimu huyo anakuwa salama.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Katavi, Ernest Hinju alidai kuwa suala hilo lipo ofisini kwake na wameanza kulitafutia ufumbuzi. “Jambo hili linahitaji ushirikishwaji wa vyombo mbalimbali ikiwemo Bodi ya Shule ya Sekondari ya Usevya,” alieleza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa katika ziara mkoani Katavi mwezi uliopita, mke wa mwalimu Ng’oka alitinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini Maji Moto akiwa na bango lenye malalamiko ya kutishiwa usalama wa maisha wa familia yake, na Waziri Mkuu alimwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa kushughulikia malalamiko hayo.
DIAMOND Msamehe Baba'ko, Mbona Q-Chief Aliweza?
Ni kweli inauma mno kutelekezwa na mzazi. Mimi ambaye baba na mama yangu walinilea kwa umoja wao pamoja na umaskini wetu, huwa nawaza ingekuwaje baba au mama asingekuwa karibu yangu? Malezi ya mzazi mmoja au wote wasingekuwepo. Inaumiza sana!Hiyo ndiyo sababu naweza kuhisi kile ambacho kinamuumiza mtoto aliyetelekezwa. Mimi ni baba, najua ni kiasi gani mtoto wangu ananihitaji kwa ukaribu. Upendo wangu kwake umekuwa zawadi yake muhimu kutoka kwangu kuliko kitu chochote. Hivyo basi, najua atapitia machungu kiasi gani kama nikimtelekeza.
Chukua hii; Kwa hali yoyote ile, mzazi hana leseni ya kumtelekeza mtoto wake. Changamoto zije na ziondoke, hakikisha unabaki umemganda mwanao. Kosa la kumtelekeza mtoto linafanana na la kuua. Huyo ni mtoto wako, unamkimbia, unataka alelewe na nani?
Mwanamuziki Aboubakar Shaban Katwila ‘Q Chilla’ katika nyimbo zake Aseme na Si Ulinizaa, alionesha wazi kuumizwa na alivyokataliwa na baba yake, Shaban Katwila, tangu akiwa mimba.
Baba mcheza soka maarufu Tanzania, mtoto anaishi kwa shida, akisaidiwa na wasamaria wema, wakati huo mama mzazi alishafariki dunia. Q Chilla akaokotwa! Ukitafakari vizuri unaweza kuhisi Q Chilla aliumia kiasi gani.
Baada ya vilio vingi, mzee Katwila alitumia njia mbalimbali kutengeneza suluhu na mwanaye. Wakasameheana na kudumisha upendo kama mtu na mzazi wake. Tangu hapo, Q Chilla alipitia vipindi vingi vibaya, baba yake akawa msaada wake.
Mara ya mwisho nilipozungumza na Q Chilla, alikiri kuwa yupo kwenye kipindi kizuri sana cha maelewano na baba yake na kwamba alikuwa mmoja wa watu waliompigania aweze kuacha matumizi ya dawa za kulevya baada ya kutopea.
Chukua hii; Watu hufanya makosa lakini ni haohao hugeuka watu wazuri. Anaweza kukutenda leo lakini kesho akakufaa. Ni mwongozo wa wahenga kuwa hupaswi kutupa jongoo na mti wake.
Isisahaulike migogoro ya kimapenzi husababisha maumivu mengi kwa watoto, vilevile uchonganishi kati ya mtoto na mzazi mmoja. Mama akibaki na mtoto baada ya kutofautiana na baba yake, anaweza kumjaza mtoto sumu kuwa baba yake alimsusa, hakumjali.
Hutokea kwa akina baba ambao hulea watoto bila mama zao, nao hutema sumu yenye uchonganishi kati ya mtoto na mama yake. Ni vizuri sana mtoto anapopevuka ayapime matukio ya nyuma kwa kutumia akili ya kikubwa. Anaweza kupata majibu ambayo ni mazuri mno kwa maisha yake.
Kwanza mzazi ambaye anamtelekeza mtoto wake ni mtu ambaye anastahili mno kuhurumiwa, maana hawezi kuwa sawasawa. Binadam aliyekamiliki kiakili anatambua kuwa mtoto ni sehemu ya maisha yake, hatathubutu kumtelekeza.
Stadi wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ ana machungu yake. Alishapata kueleza kuwa baba yake, Abdul Juma hakuwa na muda naye kipindi anakua, hivyo jukumu la malezi na ukuaji wake, lilisimamiwa na mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra Khan’.
Malezi ya Diamond yalijaa machozi na jasho, mama yake akihangaika huku na huko kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji muhimu, japokuwa haikuwezekana kupata yote. Kwamba wakati huo wa mateso, baba yake aliendekeza utoto wa mjini, akashindwa kuzingatia kuwa yeye ni baba.
Diamond naye ameamua kutoa adhabu kali kwa baba yake. Hamshirikishi kwenye mafanikio yake. Wengi tu wanakula matunda ya kazi yake ya muziki ambayo imempa umaarufu mkubwa barani Afrika na kwingineko duniani, baba mtu haambulii chochote.
Baba Diamond anapigika, anaumwa anakosa mpaka msaada wa matibabu, wakati huo Diamond anatapanya fedha kwa watu wengine. Inawezekana anafanya hivyo kutokana na hasira kali alizonazo, ila zimezidi kipimo.
Leo hii Diamond hana ubavu wa kumfuta baba yake kwenye mzunguko wa maisha yake, isipokuwa atabaki kuwa baba yake anayemchukia. Na je, hizo chuki hazifiki mahali zikaisha?
Kuna adhabu kubwa ambayo Diamond anashindwa kuitumia, na yenyewe ni kuwa chanya kwa baba yake. Angekuwa anamjali na kumpa huduma nyingi muhimu, angekuwa anamsuta kwa vitendo, kwamba yeye alimtelekeza kisha anamhudumia.
Uamuzi wa Diamond kutomjali baba yake ni kisasi. Na ni mwendelezo wa damu mbaya ambayo mara nyingi huhama kutoka kwa mzazi mmoja kwenda kwa mwingine.
Leo hii Diamond ni baba, yupo vizuri na mwanaye kwa sababu hakuna mgogoro kati yake na mama wa mtoto wake ambaye pia anatarajia kumzalia mtoto wa pili. Mama ni raia wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mtoto aliyepo ni wa kike, Latiffah, wanatarajia wa kiume.
Inaweza kutokea baadaye Diamond akagombana na Zari kisha akawa mbali na watoto wake kwa sababu ni wadogo. Mama akatumia nafasi yake kuwajaza sumu watoto wake kuwa baba yao aliwatelekeza. Nao wakikua wakamchukia baba yao. Diamond anatakiwa ayapime hayo.
Huu ni wakati mzuri mno kwa Diamond kukata mnyororo wa chuki kati yake na baba yake. Kutosikia kilio cha baba yake ambaye anaumwa ugonjwa mkubwa (kansa), ni roho ngumu mno. Ni roho ngumu mithili ya ile ya Jenerali Idd Amin Dada wa Uganda.
Diamond anayo nafasi ya kumhudumia baba yake kama ambavyo mtu anaweza kujitolea kwa ajili ya raia wengine wenye matatizo wanaomgusa. Kiusamaria wema tu. Ajitolee tu!
Namkumbusha kuwa alimnunulia gari aliyekuwa mkongwe wa muziki nchini, marehemu Marehemu Muhidin Maalim Gurumo, baba yake akiwa anaishi katikati ya dhiki kubwa. Vilevile amekuwa akinukuliwa kutoa misaada mbalimbali, baba yake anateseka. Misaada sharti ianze nyumbani.
Hiyo chuki mpaka lini Diamond? Mbona hujakana kutumia jina lake? Unaitwa Nasibu Abdul Juma, huyo Abdul Juma unamwacha anataabika kwa sababu ya visirani vya nyakati za giza. Tafadhali Diamond usiwe na roho ya Idd Amin, haikufai. Zipo baraka nyingi utaongezewa baada ya suluhu yako na baba yako.
Imeandikwa na Luqman Maloto